Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kuwa wachezaji waliokuwa wamekwama DR Congo, tayari wamerejea nchini na kuingia kambini kuendelea na maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly
Simba imeingia kambini leo wachezaji wakirejea kutoka kanda ya ziwa ambako jana walicheza mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United na kuibuka na ushindi wa bao 1-0
"Wachezaji wetu waliokuwa wamekwama nchini DR Congo wamewasili nchini na tayari wamejiunga kambini na wenzao kwa ajili ya TOTAL WAR A POINT OF NO RETURN," amesema Manara
Wachezaji waliokuwa wamekwama ni Jonas Mkude, Rally Bwalya, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni na Ally Salum
ADVERTISE HERE