Tunao uwezo wa kuwafunga Al Ahly - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Feb 2021
Tunao uwezo wa kuwafunga Al Ahly - Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara, amesema pamoja na kutambua ugumu wa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya mabingwa watetezi Al Ahly, Simba inao uwezo wa kuifunga Al Ahly katika mchezo utakaopigwa Jumanne ijayo ndani ya dimba la Benjamin Mkapa

Akizungumza na wanahabari katika Mkutano uliofanyika Hoteli ya Serena mapema leo, Manara amesema Simba tayari wamewafunga Al Ahly walipokutana hapa jijini Dar es salaam miaka miwili iliyopita, wana kila sababu ya kurudia kile walichokifanya mwaka 2018/19

"Mara ya mwisho tulikutana hapa Dar es Salaam tukawafunga goli 1-0 kwenye mechi tuliyosema YES WE CAN na tukaweza"

"Al ahly mara zote tukicheza Tanzania tunawafunga.Tunao uwezo wa kuwafunga tena, tunao uwezo wa kushinda mechi hiyo"

"Dhamira hiyo ipo kwa kila Mwanasimba kuanzia wachezaji, benchi la ufundi, viongozi, wanachama na mashabiki wote"

"Al Ahly sio timu nyepesi. Tunaposema tunaweza kuwafunga tunajua ukubwa wao, lakini Simba hupenda mechi kubwa kama hizi"

"Mechi ya mwisho tuliita WAR IN DAR, mechi ya jasho na damu ndani ya dakika 90 na sasa tunasema TOTAL WAR : POINT OF NO RETURN hii sasa ni vita kamili ya ndani ya uwanja," amesema

Aidha Manara ametaja muda wa mchezo huo kuwa utaanza saa kumi kamili jioni

"Mechi itapigwa saa 10:00 jioni siku ya Jumanne Februari 23, 2021. Ni mechi kubwa sana kwa Simba, Tanzania na Afrika Mashariki"

Idadi ya mashabiki ambao wataruhusiwa kuushudia mchezo huo ni 30,000 tu, Manara ametaja viingilio vya mchezo huo

"CAF wametwambia wanaruhusu watu 30,000 pekee. Kwa timu kubwa kama Simba SC na Al Ahly kiingilio cha Mzunguko - Tsh. 3,000 ukibaki nyumbani Usimba wako ni wa mashaka. 15,000 - VIP B, 30,000 - VIP A . Viingilio hivi mwisho Jumatatu usiku. Ikiingia Jumanne Mzunguko - Tsh. 5,000, VIP B - 20,000 na VIP A - Tsh. 40,000"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’