Baada ya kufanikiwa kusonga mbele katika mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika, Kocha Msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, amesema kuwa kikosi chake kitalazimika kuhakikisha wanatumia vizuri dakika 90 za nyumbani kwenye mchezo ujao dhidi ya Al Masry kupata ushindi.
Simba imetinga hatua ya awali ya michuano hiyo baada ya kuifunga Gendarmarie Nationale FC ya Djibouti mabao 5-0, ilipata ushindi mnono nyumbani wa magoli 4-0 huku juzi ilipokuwa ugenini ilishinda bao 1-0.
Djuma amesema kuwa wanahitaji kupata ushindi katika mchezo wa kwanza ili kuondoa presha katika mechi ya marudiano na mipango ya kuhakikisha wanatimiza malengo yao utaanza kwenye mazoezi leo.
"Tutaingia uwanjani kama vile hakuna mechi ya marudiano, tunataka kuona tunashinda katika mechi ya kwanza ili mchezo wa marudiano usiwe wenye mawazo na kuhitaji nguvu ya ziada, naamini Mungu atatusaidia kufikia malengo yetu," alisema Djuma, kocha wa zamani wa Rayon Sports ya Rwanda.
Kikosi cha Simba kimerejea nchini jana usiku kikitokea Djibouti na leo kitaanza mazoezi rasmi ya kujiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbao FC
"Baada ya mechi ya jana (juzi) timu yetu jana asubuhi ilianza mazoezi na itarejea nyumbani leo (jana) usiku, pia ninapenda kuwaambia kuwa CAF (Shirikisho la Soka Afrika) wamethibitisha kuwa tunaanzia nyumbani Jumanne.Machi 6 na mchezo wa marudiano ni Ijumaa Machi 16, kwangu mimi hii ni faida kwa sababu hata mwaka 1993 tulipofanya vizuri tulianzia nyumbani halafu unawafuata kwao," alisema Haji Manara, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba.
Manara aliongeza kuwa benchi ya ufundi linatarajia kutumia mechi za Ligi Kuu kama sehemu ya kujiimarisha na mchezo huo dhidi ya Al Masry kwa sababu wanahitaji kushinda taji la Bara msimu huu.

ADVERTISE HERE