Mabingwa wa nchi sasa wanaweza kurejea katika nafasi yao bila ya 'longolongo' kama watashinda mechi zao zote za viporo
Wakiwa nafasi ya pili na alama zao 39, wakishinda michezo yao mitatu watafikisha alama 48 ambazo ni alama mbili zaidi ya Yanga ambayo leo imekamatwa na wababe wao Kagera Sugar na kuambulia sare ya mabao 3-3
Simba wako Musoma na watashuka uwanjani kesho Alhamisi kuikabili Biashara United
Huu ni mchezo ambao 'Mnyama' anahitaji alama zote tatu ili kuhakikisha anarudi katika nafasi yake mapema zaidi
Mbio za sakafuni huishia ukingoni, taratibu naona 'uto' wameanza kukata pumzi...!
ADVERTISE HERE