Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) limeagiza kuwa michezo yote miwili ya kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho kati ya CD de Agosto ya Angola dhidi ya Namungo, itapigwa nchini Tanzania
CAF imeagiza michezo hiyo kupigwa kabla ya Februari 26 2021
CAF iliufuta mchezo wa kwanza baina ya timu hizo uliopaswa kupigwa Februari 14 nchini Angola kutokana na kadhia ambazo kikosi cha Namungo Fc kilipata kutoka kwa mamlaka za Serikali ya Angola juu ya changamoto ya corona
Mpaka sasa wachezaji watatu wa Namungo Fc na CEO wao bado wako Angola baada ya vipimo vyao kuonyesha kuwa na maambukizo ya virusi vya corona
Timu nzima ya Namungo iliwekwa kizuizini mamlaka zikitaka msafara wote uwekwe karantini kwa siku tatu
CAF ikaufuta mchezo huo na kuagiza wachezaji na viongozi wa Namungo Fc ambao hawakukutwa na maambukizi ya corona waruhusiwe kurejea nchini