Milton atamba ubora wa makipa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Feb 2021
Milton atamba ubora wa makipa Simba

Kocha wa makipa wa klabu ya Simba, Milton Nienov, amesema viwango vya makipa wote watatu wa Simba kwa sasa viko juu, tofauti na mwanzo alivyokuja

Akizungumza jijini Dar es Salaam, kocha huyo Mbrazil ambaye alijiunga na Simba mwanzoni mwa mwaka huu, alisema makipa wote aliuowakuta kwenye kikosi hicho ni wazuri, lakini alichofanya ni kuwaongezea mbinu ambazo zitawafanya waonekane bora.

Simba ina makipa watatu ambao ni Aishi Manula, Beno Kalolanya na Ally Salim.

"Hakijaongezeka kwa Manula tu, au kwa Kakolanya, ila hata kwa Ally, naye ameongezeka kiwango na kama akipata nafasi ataonyesha kile ambacho amekipata," alisema kocha huyo.

Mashabiki wengi wa soka nchini kwa sasa wameonekana kukoshwa na kiwango cha hali ya juu cha Manula akiwa na Simba pamoja na timu ya Taifa, Taifa Stars.

Manula ambaye kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika amecheza mechi nne bila wavu wake kutikiswa, lakini alitia fora kwenye Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zilizomalizika hivi karibuni nchini Cameroon.

Kwa miaka ya hivi karibuni, Manula alikuwa akituhumiwa kushuka kiwango kwa kuruhusu mabao rahisi akiwa kwenye timu ya taifa na hata akiwa na Simba.

Na hii ilisababisha hata viongozi wa Simba, pamoja na mambo mengine, kubadilisha kocha wa makipa ambaye wakati huo alikuwa Mwarami Mohamed, kabla ya kumtwaa Mbrazil huyo.

Manula hakufungwa kwenye mechi za awali kati ya Simba dhidi ya Plateau United, timu yake ikishinda bao 1-0 ugenini na suluhu nyumbani, ikishinda mabao 4-0 nchini Tanzania dhidi ya FC Platinum ya Zimbabwe, na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya AS Vita ya DR Congo.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
50m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’