Kila la kheri Ngorongoro Heroes michuano ya Afcon U20

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Feb 2021
Kila la kheri Ngorongoro Heroes michuano ya Afcon U20

Ngorongoro Heroes timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 iko Mauritania kushiriki michuano ya Afcon u20

Heroes leo wanashuka dimbani kuikabili Ghana katika mchezo wao wa kwanza kundi C utakaopigwa kuanzia saa moja usiku kwa saa za Tanzania

Vijana hao wa Tanzania wako kundi C wakiwa pamoja na Ghana, Morocco na Gambia

Kundi hili ndilo linalotizamwa kama kundi la kifo

Pamoja na michuano hiyo kuwa na faida kwa nchi, vijana wenyewe watanufaika kwani watakuwa na nafasi ya kuonekana na Mawakala wa soka duniani kote

Na ikitokea wakafanya vizuri na hata kutinga nusu fainali, watapata nafasi ya kwenda kushiriki michuano ya kombe la dunia la vijana

Mchezo wa leo dhidi ya Ghana ni muhimu sana kwao kuanza vyema

Kocha wa timu hiyo Jamhuri Kiwhelo 'Julio' amesema vijana wake wako tayari kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo pamoja na kuwa wanakutana na wapinzani ambao wana wachezaji 'vijeba'

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
13h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
13h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
16h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’