Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kinaondoka jioni ya leo Jumanne kuelekea Mwanza na kesho kuunganisha mkoani Mara kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United ambao utapigwa keshokutwa Alhamisi katika uwanja wa Karume
Simba itaondoka na ndege mpaka jijini Mwanza ambako mabingwa hao wa nchi wataweka kambi ya siku moja na kesho Jumatano kuelekea mkoani Mara
"Kikosi cha mabingwa wa nchi leo jioni kitaondoka kwa ndege jijini Dar es Salaam kwenda jijini Mwanza na kesho Jumatano kitaelekea mkoani Mara ambako kitacheza mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Biashara United siku ya Alhamisi Februari 18, 2021 kwenye uwanja wa Karume," imesema taarifa iliyotolewa na Simba mapema leo
ADVERTISE HERE