Mugalu ataja siri ya kuwatungua AS Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Feb 2021
Mugalu ataja siri ya kuwatungua AS Vita

Mshambuliaji wa Simba Chris Mugalu amekuwa na rekodi nzuri ya kupachika mabao kila anapokutana na klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Bao la mkwaju a penati alilofunga juzi na kuipa Simba ushindi muhimu wa bao 1-0 katika michuano ya ligi ya mabingwa, ni mwendelezo wa kazi ambayo amekuwa akiifanya kila anapokutana na AS Vita

Mugalu amefuichua kuwa ameifunga AS Vita akiwa na vilabu vitatu tofauti na jambo hilo linasukumwa na kiu yake ya kutaka kuitwa kuitumikia timu ya Taifa ya DR Congo ambayo inafundishwa na Florente Ibenge anayeinoa AS Vita

"Nimekuwa na rekodi nzuri ya kufunga kila ninapokutana na AS Vita, hili jambo ambalo nimejiwekea kila mara ninaposhuka dimbani kucheza nao"

"Ninayo ndoto ya siku moja kuitumikia timu yangu ya Taifa hivyo kwangu mechi dhidi ya AS Vita ni fursa hasa ikizingatiwa wanafundishwa na Ibenge ambaye hufundisha timu ya Taifa"

"Niliwafunga wakati nacheza Fc Lupopo hapa Congo na hata nilipokwenda Zambia klabu ya Lusaka Dynamos, tulipokuja hapa niliwafunga. Na sasa nimewafunga tena nikiwa na Simba"

"Mara nyingi nimemshawishi Ibenge aweze kuniita timu ya Taifa bila ya mafanikio lakini naamini wakati huu anaweza kuniita kwani nimetimiza majukumu yangu vyema. Lakini pia kucheza hapa DR Congo ni rahisi kwangu sababu niko nyumbani. Nimecheza mara nyingi katika uwanja huu (stade de Martyrs), hivyo nilitaka kuwaonyesha watu wa hapa nyumbani kuwa bado niko vizuri pengine zaidi ya vile walivyoniona mwanzo," alisema Mugalu

Pamoja na kufunga bao pekee, Mugalu alionyesha kiwango kizuri katika mchezo huo uliopigwa usiku wa Ijumaa ya wiki iliyopita

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’