Gikanji aitabiria Simba kufika mbali ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Feb 2021
Gikanji aitabiria Simba kufika mbali ligi ya mabingwa

Kiungo fundi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Doxa Gikanji maeitabiria Simba kufanya vizuri katika michuano ya ligi ya mabingwa mwaka huu baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita ugenini

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, anatarajiwa kujiunga na Simba mwezi Juni baada ya mchakato wa usajili wake kukwama kwenye dirisha dogo kutokana na kuwa na majukumu ya timu ya Taifa ya DR Congo iliyokuwa ikishiriki michuano ya CHAN ilifanyika Cameroon

Wakati Simba ikiwa DR Congo kwa ajili ya mchezo dhidi ya AS Vita, Gikanji alipata nafasi ya kuonana na viongozi pamoja na wachezaji wa Simba akiwapongeza baada ya ushindi huo

Gikanji anayeitumikia DC Motema Pembe, amesema Simba ina nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa na wanaweza kufanya hivyo wakiwa na mechi mkononi

"Kikosi cha Simba kiko imara sana, nadhani kama watacheza hivi kwa mechi zao za nyumbani wanaweza kushinda zote. Na pia wana nafasi ya kupata alama nyingine ugenini, nafikiri wanaweza kufikisha alama 12 au zaidi na kuwa na uhakika wa kumaliza kwenye nafasi ya kwanza au ya pili"

"Sioni kama Simba wanaweza kushindwa kusonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano hii," Gikanji alinukuliwa na Mwanaspoti

Gikanji alipaswa kuwa katika kikosi cha Simba kinachoshiriki ligi ya ndani lakini ushiriki wake wa michuano ya CHAN ulikwamisha usajili wake kwani ili asajiliwe na Simba alipaswa kuondoa jina lake kwenye kikosi cha DR Congo ambacho kilikuwa kimetinga robo fainali

Michuano ya CHAN ilihusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani yeye kusajiliwa na Simba ingemuondolea sifa ya kushiriki michuano hiyo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’