Mzamiru ni shujaa asiyeimbwa sana

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Feb 2021
Mzamiru ni shujaa asiyeimbwa sana

Kama kuna mchezaji ambaye hazungumzwi sana katika kikosi cha Simba licha ya kazi kubwa anayofanya dimbani, basi ni Mzamiru Yassin

Huu ni mwaka wake wa nne yuko ndani ya kikosi cha Simba lakini mara chache utawasikia hata wachambuzi wa soka nchini wakimzungumzia

Ni kwa sababu Mzamiru hupewa majukumu maalum uwanjani, na huwatengenezea wachezaji wengine waweze kun'gara

Shiza Kichuya, kiungo wa zamani wa Simba ambaye alianza kucheza na Mzamiru tangu wako Mtibwa Sugar, aliwahi kusema kwake Mzamiru ni mchezaji aliyekamilika sana kuliko wachezaji wengi

Wakati huo Simba ilikuwa na changamoto katika safu yake ya ulinzi, Kichuya alitamani kuona Mzamiru akipewa majukumu katika safu hiyo kwani aliamini Mzamiru anaweza kucheza popote

Wengine wamempachika jina la utani 'punda', tunafahamu kazi kubwa ya punda ni kubeba mizigo kumrahisishia msafiri hasa maeneo ya Jangwani kwenye ukame

Huo ni mfano wa kazi ambayo Mzamiru huifanya pale Simba. Ni mchezaji ambaye utamuona muda wote akiwajibika uwanjani, huyu bwana ana mapafu ya mbwa!

Juzi Simba ilipata ushindi kule DR Congo katika mchezo wake wa kwanza ligi ya mabingwa hatua ya makundi kwa kuifumua AS Vita bao 1-0

Mzamiru alikuwa mtu muhimu sana katika eneo la kiungo cha ulinzi akishirikiana vyema na Injinia Taddeo Lwanga ambaye kwa hakika ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’