Ushindi wa Simba DR Congo umeingia kwenye rekodi za CAF

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Feb 2021
Ushindi wa Simba DR Congo umeingia kwenye rekodi za CAF

Ushindi wa bao 1-0 iliyopata Simba dhidi ya AS Vita juzi kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi, umeingia katika rekodi ya Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) ukiwa ni ushindi wa kwanza wa ugenini kwa Simba na klabu ya kwanza Tanzania katika hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

"Hii ni Simba, ushindi wa kwanza ugenini kwenye historia ya Ligi ya Mabingwa Afrika ngazi ya makundi." liliandika Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye mtandao wake wa kijamii kwa lugha ya Kiingereza, likiielezea timu ya Simba na ushindi wake wa bao 1-0 ilioupata dhidi ya AS Vita

Kwa hakika ni ushindi ambao umeonekana pamoja na kuwafurahisha Watanzania wengi, lakini pia umewashangaza baadhi ya mashabiki wa soka Afrika, kwani ni nadra kwa AS Vita kufungwa kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Kwa ushindi huo, Simba imeweka rekodi ya kufunga mabao sita na kufungwa bao moja, huku ikicheza bila kuruhusu bao lolote kwenye mechi nne ilizocheza tangu kuanza kwa Ligi ya Mabingwa msimu huu.

Ilianza safari yake kwenye mechi ya awali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwa kuichaa bao 1-0 ugeini na mechi ya marudiano nchini ilimalizika bila kufungana.

Kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ilichapwa bao 1-0 ugeini dhidi ya FC Platinum, lakini ikashinda mabao 4-0 mechi ya marudiano, kabla ya kuanza kwa kushinda bao 1-0 dhidi ya AS Vita hatua ya makundi.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
34m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’