Kocha Mkuu wa AS Vita Florente Ibenge amekiri kuwa timu yake ilizidiwa mbinu na Simba kwenye mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi, uliopigwa jijini Kinshasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Simba kuondoka na ushindi wa bao 1-0
Ibenge amesema wachezaji wake walishindwa kuivuka ngome ya safu ya ulinzi ya Simba ambayo wachezaji walicheza pamoja kwa muda wote
Aidha amewapongeza mabingwa hao wa nchi kwa kuondoka na alama zote tatu huku akieleza kuwa wanajipanga kufanya vizuri katika michezo yao mingine
"Hatukuwa bora dhidi ya wapinzani wetu, Simba walifahamu namna gani ya kucheza na sisi wakiwa ugenini, hivyo ubora wa wachezaji wangu ulikuwa chini katika kupangua mbinu za Simba"
"Nawapongeza wapinzani wetu kwa hilo lakini bado kuna safari ndefu japo si njema kupoteza tukiwa nyumbani, tunahitaji kuboresha ili tujiweke katika nafasi nzuri," alisema Ibenge
Inaelezwa baada ya kipigo hali si shwari ndani ya AS Vita Ibenge na benchi lake la ufundi wakishinikizwa wajiuzulu