Tangu jana klabu ya Namungo Fc, Wawakilishi wengine wa nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho, wamekwama nchini Angola walikokuwa wamekwenda kucheza na CD de Agosto mchezo wa kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo
Mamlaka za nchi hiyo zilieleza wachezaji watatu wa Namungo Fc kudaiwa kukutwa na corona pamoja na Mtendaji Mkuu Omary Kaya
Mamlaka nchini Angola ziliiweka Namungo Fc kizuizini huku wakishinikiza timu nzima iwekwe karantini kwa muda wa siku tatu wakati mchezo husika ulipaswa kupigwa kesho
Sasa CAF imetangaza kufuta mchezo huo, Maamuzi ya mwisho kuhusu hatma yake yakisubiri kikao cha Kamati husika

ADVERTISE HERE