Hivi karibuni kumeibuliwa tetesi kwenye mitandao ya kijamii zinazodai kuwa mlinzi wa kati wa Simba Paul Bukaba ni raia wa Burundi.
Bukaba alisajiliwa Simba kama Mtanzania licha ya kuwa alisajiliwa kutoka Atletico Olympic aliyocheza kwa muda mrefu nchini Burundi.
Manara amefafanua kuwa Bukaba ni Mtanzania wa kuzaliwa na alikwenda Burundi kucheza mpira.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Manara ameandika;
"Tunazo taarifa za hovyo zinazosambazwa eti mchezaji wetu Paul Bukaba ni Mrundi na hvyo tutakatiwa rufaa dhidi ya Wadjibout.
"Poul Bukaba @bukaba_paul ni Mtanzania na Burundi alienda kucheza Soka tu na anamiliki uraia wa kuzaliwa wa Tanzania," amefafanua Manara
"Tafuteni lingine hili mmenoa na pia hangaikeni na yenu ikiwemo kulipa mishahara ya wachezaji wenu"
Walioanzisha 'zengwe' hilo wanaituhumu Simba kuwa imesajili wachezaji nane wa Kimataifa tofauti na kanuni za shirikisho la soka nchini (TFF) zinazotaka wachezaji wa Kimataifa wasizidi saba.

ADVERTISE HERE