Katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Simba ni mwendo wa kuweka rekodi tu
Jana wakiwa wamevaa uzi unaolitangaza Taifa la Tanzania (Visit Tanzania), mabingwa hao wa nchi walipeperusha vyema bendera ya Tanzania kule DR Congo wakifanikiwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya AS Vita
Ni ushindi ambao umewashuhudia wababe hao wa soka nchini wakiongoza kundi A wakiwa na alama tatu
Ushindi huo unaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kwani Simba imekuwa klabu ya kwanza kushinda katika michuano ya ligi ya mabingwa huko Congo
Simba walifanya hivyo katika hatua ya awali ya michuano hiyo wakipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United ya Nigeria na kuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kushinda ndani ya ardhi ya Nigeria
Lakini pia Simba imekuwa klabu ya kwanza kushinda ugenini mchezo wa hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa
Halafu huko mtaani utasikia kuna watu wanasema Tanzania kuna timu kubwa kuliko Simba?
Huku ni kuwakosea heshima mabingwa hawa wa Taifa hili, timu nyingine hapa Tanzania zinapaswa kujifunza kutoka kwa Simba