Injinia Taddeo Lwanga, huyu ndio mkata umeme sasa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Feb 2021
Injinia Taddeo Lwanga, huyu ndio mkata umeme sasa

Moja ya sajili ambazo uongozi wa Simba unajivunia ni pamoja na huyu mwamba kutoka nchini Uganda Injinia Thadeo Lwanga

Wakati anaanza kuitumikia Simba kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi wapo waliombeza

Lakini sasa ni wazi Lwanga amedhihirisha ni aina ya mchezaji ambaye Simba ilimuhitaji sana katika kuimarisha safu yake ya ulinzi pamoja na kuwa yeye ni kiungo mkabaji

Kazi kubwa aliyoifanya kwenye mchezo dhidi ya AS Vita kule DR Congo, imedhihirisha umuhimu wake katika kikosi cha Simba

Hana mambo mengi anapokuwa uwanjani, anafahamu sana majukumu yake na wakati wote yuko eneo sahihi

Kiwango alichoonyesha kwenye mchezo dhidi ya AS Vita ambao Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0, kinastahili kupewa tuzo ya nyota wa mchezo

Lwanga alivuruga mawasiliano ya eneo la ushambuliaji la As Vita kwani wakati wote alifika maeneo kuwatibulia mipango

Sasa kocha Didier Gomes ana mtu makini katika eneo lake la kiungo cha ukabaji. Tunaweza kushuhudia Jonas Mkude akisogezwa mbele zaidi kwani Lwanga ameonyesha kuwa yeye ni bora zaidi katika kukaba ukimlinganisha na Mkude

Lwanga ni moja ya sajili bora sana iliyofanywa na Simba dirisha dogo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’