Mabingwa wa nchi Simba wako DR Congo usiku wa leo wakitarajiwa kushuka Stade de Martyrs kuikabili AS Vita katika mchezo wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi
Mchezo huu utaruka hewani kuanzia saa nne kamili usiku kwa saa za Tanzania ambapo kule DR Congo itakuwa saa mbili usiku
Ni msimu mwingine wa michuano hii mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu, matumaini ya mashabiki ni kuona Simba leo inaanza na matokeo mazuri katika mchezo wake wa kwanza
Kikosi cha kocha Didier Gomes kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo jana usiku wakikamilisha maandalizi ya mwisho
Katika Mkutano na Waandishi wa habari, Msemaji wa Simba Haji Manara alisema wanaiheshimu AS Vita kwa sababu ni klabu kubwa lakini hawana uwoga wowote kucheza nao
Aidha amesema Simba sasa iko imara zaidi ukilinganisha na mara ya mwisho walipocheza dhidi ya AS Vita na kufungwa mabao 5-0
Ni mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali kwani kila timu itahitaji kuanza michuano hiyo vizuri
Hakuna shaka, Wawakilishi wa nchi Simba watawatoa 'kimasomaso' mashabiki wa Simba na Watanzania kwa kupata matokeo mazuri leo
Kila la kheri Simba, kila la kheri Mnyama...!