Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema anatarajia mchezo mkali wenye ushindani kutoka kwa AS Vita siku ya kesho timu hizo zitakapokutana katika mchezo wa kwanza ligi ya mabingwa hatua ya makundi
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake kuelekea mchezo huo, Gomes amesema wamefanya maandalizi ya kutosha, wachezaji wake wako tayari kuwakabili AS Vita
"Utakuwa mchezo mgumu sababu Vita Club ni timu nzuri. Tuna nafasi nyingi za kupata matokeo mazuri"
"Tumejiandaa kikamilifu kucheza mchezo huu. Nimeongea na wachezaji na nimewambia kipi natarajia kwenye mchezo wa kesho. Tupo tayari na ninauhakika tunaweza kuanza vizuri mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi," amesema Gomes
Nae mshambuliaji Chris Mugalu, amesema wachezaji wote wanafahamu ugumu wa mchezo huo lakini wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri
"Haitakuwa mechi rahisi, itakuwa mechi kali na najua tutapambana. Kama tukifata ambacho kocha ametwambia naamini matokeo yatakuwa mazuri sana."
"Simba tunawachezaji wazuri na tunajiandaa na mechi ya kesho lakini haitakuwa mechi rahisi. Nawaomba Wanasimba watukumbuke kwenye maombi. DR Congo ni nyumbani na ukiwa nyumbani inatakiwa ufanye kitu kizuri," amesema Mugalu