Vita wamebanwa kila kona, wasubiri kipigo tu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Feb 2021
Vita wamebanwa kila kona, wasubiri kipigo tu

Kikosi cha Simba jana usiku kilifanya mazoezi yake ya kwanza katika Uwanja wa De Martyrs uliopo Kinshasa, DR Congo lakini katika hali ya kushangaza wakati wanaendelea na mazoezi hayo, msafara wa AS Vita ulifika katika uwanja huo kwa kile kilichoonekana kutaka kuibia mazoezi ya Simba ingawa jaribio hilo lilizimwa na viongozi wa Simba na Watanzania waishio hapa Kinshasa.

Mazoezi hayo yalifanyika saa 2.00 usiku jijini Kinshasa sawa na saa 4.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki na ghafla msafara wa AS Vita uliokua na wachezaji, maofisa wa benchi la ufundi na viongozi ulifika na kupaki basi lao nje ya uwanja huo unaoingiza mashabiki takribani 80,000.

Kitendo cha kuwasili kwa AS Vita katika muda ambao Simba walikuwa wanaendelea na mazoezi uwanjani hapo, kiliwafanya viongozi wa Simba na Watanzania wanaoishi hapa Kinshasa, kuongeza umakini na ulinzi katika kila pembe ya uwanja ambapo hawakuruhusu mtu yeyote kushuhudia mazoezi hayo hata kwa kuibia.

Iliwalazimu AS Vita kusubiri hadi Simba wamalize kufanya mazoezi yao na baada ya hapo waliingia uwanjani kwa ajili ya program zao za mazoezi

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’