Lwanga, Nyoni kupewa kazi maalum mechi ya AS Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Feb 2021
Lwanga, Nyoni kupewa kazi maalum mechi ya AS Vita

Simba imeondoka nchini Tanzania kuelekea DR Congo ikiwa na kikosi chenye wachezaji 27 ambapo Ijumaa, Februari 12 2021 watashuka dimbani kucheza mechi ya kwanza ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita

Huu ni mchezo ambao Kocha Didier Gomes atahitaji kucheza kwa tahadhari hasa ikizingatiwa yuko ugenini

Miongoni mwa wachezaji aliowajumuisha katika kikosi chake ni beki kiraka Erasto Nyoni na kiungo Jonas Mkude ambaye hakuwa na timu kwa takribani mwezi mmoja akiwa amesimamishwa kwa makosa ya utovu wa nidhamu

Wakati wote ambao Mkude amekosekana kikosini, Mganda Taddeo Lwanga, amefanya majukumu yake vyema. Kiungo huyu aliyetua Simba kwenye usajili wa dirisha dogo, tayari ameanza kuzikonga nyoyo za mashabiki wa Simba ambao wanafurahia kazi yake

Wakati Simba inaondoka jijini Dar es salaam jana, Gomes alidokeza kuwa Mkude hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani kule DRC kwa kuwa bado hayuko fiti

"Mkude ni mchezaji mzuri, lakini anahitaji kufanya mazoezi kwanza. Nilimtazama kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya timu yetu ya vijana, nafikiri hayuko tayari kwa mchezo," alisema Gomes

Hata hivyo Mfaransa huyo, alieleza kuvutiwa na mkongwe Erasto Nyoni na kuongez kuwa anaweza kuwa na msaada katika mchezo wa keshokutwa

"Nyoni yuko tayari zaidi, nafikiri anaweza kuwa na mchango wake kwenye eneo la kiungo katika mchezo dhidi ya AS Vita," alisema Gomes

Katika mchezo huo, huenda Gomes akaanza na viungo wakabaji wawili ili kuipa timu uwiano mzuri katika kujilinda kwani mchezo huo unatarajiwa kuwa na presha kubwa kutoka kwa wenyeji

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’