Msafara wa kikosi cha Simba unaojumuisha watu 44 unaondoka leo saa kumi Alasiri kuelekea DR Congo kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita ambao utapigwa Ijumaa, Februari 12 saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki
Wachezaji 27, benchi la ufundi na viongozi wataondoka na Ndege mpaka Ethiopia ambako wataunganisha moja kwa moja kuelekea DR Congo, timu ikitarajiwa kuwasili nchini humo kesho Jumatano
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema timu inaondoka nchini ikiwa na morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo wa kwanza kundi A
Manara amewataka Watanzania kuwaombea ili waweze kufika salama na kuweza kupata matokeo muhimu katika mchezo huo
Simba ilitanguliza maafisa wake kule DR Congo ambao wanaandaa mapokezi ya kikosi kuhakikisha timu inakuwa katika mazingira salama
Kila la kheri Simba, kila la kheri mabingwa, kila la kheri wawakilishi wa nchi