Baada ya kukamilisha mchezo wa kiporo dhidi ya Azam Fc hapo jana, mabingwa wa nchi Simba wanatarajiwa kuondoka nchini kuelekea DR Congo kwa ajili ya majukumu ya Kimataifa ambapo Ijumaa ya wiki hii watakuwa dimbani kuwakabili wenyeji wao AS Vita
Simba itaondoka nchini ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza wa ligi ya mabingwa hatua ya makundi
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Salim Abdallah 'Try Again' amesema wataondoka na wachezaji wote waliowasajili kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa
Kutokana na uwepo wa janga la corona, Try Again amesema watawachukua wachezaji wote kwa ajili ya tahadhari
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema mchezo dhidi ya Azam Fc umemsaidia kufanya maboresho muhimu ya kikosi chake kabla ya kuwakabili AS Vita Ijumaa