Mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Azam Fc umemalizika kwa timu hizo kugawana pointi baada ya kutoka sare ya mabao 2-2
Ni mchezo ambao wachezaji wa Simba watajilaumu wenyewe kwa kushindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza hasa kwenye kipindi cha kwanza Chama akikosa mkwaju wa penati
Aidha kwa upande mwingine Azam Fc watamshukuru mlinda lango wao Kigonyi aliyeokoa mashambulizi mengi
Meddie Kagere ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao katika mchezo huo akifunga bao maridhawa katika dakika ya 27 akimalizia krosi ya Luis Miquissone


Mabingwa hao watetezi walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0
Kipindi cha pili Simba ilipunguza kasi na kuwapa nafasi Azam Fc kurejea mchezoni
Iddi Selemani 'Nado' aliirejesha Azam Fc mchezoni kwa bao safi kwenye dakika ya 67 kabla Ayubu Lyanga hajafunga bao la pili katika ya 76
Bao hilo halikuchukua muda kwani Miquissone aliirejesha Simba mchezoni kwa bao la pili dakika mbili tu baada ya Azam Fc kushangilia bao lao
Ni mchezo ambao matokeo ya sare hayakutarajiwa lakini mwisho wa siku alama moja ni bora zaidi kuliko mchezo huo ungemalizika kwa kufungwa
Simba sasa inaelekeza nguvu zake kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita ambao utapigwa Februari 12 nchini DR Congo