Kikosi cha Simba kiko tayari kwa mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu ni mchezo ambao Simba imetawala kwa miaka minne iliyopita na bila shaka mabingwa wa nchi wataendeleza umwamba wao
Tangu mwaka 2017, Azam Fc hawajapata matokeo mbele ya Simba kwenye ligi
Wakitoka mkoani Dodoma ambako waliondoka na alama zote tatu kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji, Mabingwa wataingia uwanja wa Mkapa leo wakiwa katika msako wa alama nyingine tatu
Ni nyota wanne tu ambao hawatakuwa sehemu ya mchezo leo kutokana na sababu mbalimbali
Nahodha John Bocco atakosekana licha ya kuwa tayari ameanza mazoezi mepesi
Wengine ni Erasto Nyoni, Ibrahim Ame na Jonas Mkude ambaye hakuwa amefanya mazoezi na wachezaji wenzake kwa takribani wiki tano akitumikia adhabu
Kocha Didier Gomes atakuwa na nafasi nyingine ya kukusanya alama tatu katika mchezo wake wa pili kwenye ligi