Wanachama wa Simba leo watashiriki kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa klabu hiyo kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Swedi Mkwabi aliyejiuzulu mwaka jana
Uchaguzi huo unafanyika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Wagombea pekee kwenye uchaguzi huo ni Juma Nkamia na Murtaza Mangungu
Baada ya zoezi la uchaguzi, Wanasimba wataelekea uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia mtanange wa kukata na shoka dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa saa kumi Alasiri
Awali mchezo huo ulipangwa kupigwa saa moja usiku lakini Bodi ya Ligi ilibadilisha muda kutokana na changamoto ya miundombinu ya taa
Ni mchezo mwingine ambao Simba inahitaji kushinda ili kuzidi kusogea karibu zaidi na kileleni
Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema mchakato wa uchaguzi utakamilika mapema ili kuwawezesha wanachama kuwahi mtanange huo
Tiketi zitapatikana nje ya ukumbi wa Mkutano