Uchaguzi Simba ni kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Feb 2021
Uchaguzi Simba ni kesho

Wananchama wa klabu ya Simba kesho Jumapili watashiriki kwenye zoezi la uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti iliyoachwa wazi na Swedi Mkwabi aliyejiuzulu nafasi hiyo mwaka jana

Kamati ya Uchaguzi ya klabu ya Simba imeeleza kuwa maandalizi ya uchaguzi huo yamekamilika ambapo ni wagombea wawili Juma Nkamia na Murtaza Mangungu watachuana

Wagombea hao walianza kampeni mapema wiki hii ambapo zoezi la kampeni litafungwa leo, saa 12 jioni

"Kesho utafanyika uchaguzi wa kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Simba wa wanachama. Wagombea wawili ndio watachuana kesho Murtaza Mangungu na Juma Nkamia. Wanachama wanatakiwa kujua hao ndio watawapigia kura," alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Boniface Lihamwike katika Mkutano na Wanahabari mapema leo

Aidha Lihamwike amesema ili Mwanachama aruhusiwe kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe amelipia ada ya uanachama wakeΒ 

"Moja ya kigezo cha kupiga kura ni mwanachama kulipia ada ya uanachama hivyo kesho nje ya ukumbi wa mkutano kutakuwa na eneo maalumu ambalo watatumia wanachama ambao hawajalipa kufanya malipo"

Mkutano Mkuu unatarajiwa kuanza saa tatu asubuhi ili ukamilike mapema Wanachama waweze kuwahi mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa kuanzia saa moja jioni

Tiketi za mchezo dhidi ya Azam zitauzwa nje ya ukumbi wa mkutano na vituo vilivyotangazwa jana

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’