Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amewapongeza wachezaji wake kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi muhimu wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri
Ukiwa ni mchezo wake wa kwanza kwenye ligi, Gomes amesema ulikuwa mchezo mgumu lakini muhimu kwao ni kuondoka na alama tatu ambazo zimewafanya wazidi kumkaribia yule aliyeko kileleni
"Ulikuwa mchezo mgumu lakini tulijua kabla ya mechi kwamba ingekuwa ngumu. Tumeridhishwa sababu lengo kuu leo ilikuwa ni kupata alama tatu na kupunguza alama zilizopo na timu inayoongoza ligi," alisema Gomes baada ya mchezo huo
Mabao ya Meddie Kagere na Bernard Morrison ndiyo yaliyoihakikishia Simba alama tatu muhimu zilizowafanya wafikishe alama 38
Simba sasa inarejea jijini Dar es salaam tayari kwa mchezo mwingine wa kiporo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa