Kiporo kimeliwa, FT Dodoma Jiji 1-2 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Feb 2021
Kiporo kimeliwa, FT Dodoma Jiji 1-2 Simba

Wenye nafasi yao pale juu wanazidi kusogea baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa uwanja wa Jamhuri Mkoani Dodoma

Hapa tunawazungumzia mabingwa wa nchi Simba kwani baada ya ushindi huo wamefikisha alama 38 sasa wakihitaji alama sita tu kutoka mechi mbili za viporo wakae kileleni

Simba walianza taratibu mchezo huo, walikuwa wa kwanza kuhesabu bao la kuongoza kwenye dakika ya 31 kupitia kwa Meddie Kagere 'MK14' aliyemalizia krosi murua iliyochongwa na Wakili Msomi Bernard Morrison 'Mzee wa Kuwakera'

Pamoja na kutokuwa na mchezo mzuri sana leo lakini Morrison ndiye aliyeihakikishia Simba alama tatu muhimu akifunga bao la ushindi kwemye dakika ya 66

Dodoma Jiji walifunga bao lao pekee kwenye dakika ya 36 kupitia mpira wa kichwa uliopigwa na Cleofas Mkandala

Ni alama tatu muhimu ambazo Simba wameondoka nazo Dodoma na sasa wanarejea jijini Dar es salaam kwa ajili ya mchezo dhidi ya Azam Fc ambao utapigwa Jumapili

Huu ni ushindi wa kwanza kwa Kocha Didier Gomes katika ligi kuu ya Vodacom

Aidha Kagere amefikisha mabao nane akikaa kileleni kwenye vita ya kuwania kiatu cha dhahabu wakilingana na mshambuliaji mwenzake wa Simba nahodha John Bocco ambaye pia ameweka kambani mabao nane

Tutaelewana tu....!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’