Wekundu wa Msimbazi, Simba wamefuzu raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kuichapa Gendarmerie bao 1-0 katika mchezo uliopigwa huko Djibouti.
Simba imefuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0 kufuatia ushindi wake wa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye dimba la Taifa wiki iliyopita.
Bao pekee la Simba leo liliwekwa kimiani na mshambuliaji Emanuel Okwi katika dakika ya 53 ya mchezo.
Simba sasa itaikabili El Masry kutoka nchini Misri baada ya timu hiyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-2, yenyewe leo imechapwa mabao 2-1 na Green Buffaloes.
Kwenye mchezo wa kwanza ilishinda kwa mabao 4-0

ADVERTISE HERE