Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba Sc jioni ya leo kitashuka katika dimba la Jamhuri mkoani Dodoma kupepetana na Dodoma Jiji ukiwa ni mcheo wa ligi kuu ya Vodacom
Baada ya mapumziko ya takribani mwezi mmoja kupisha michuano ya CHAN, ligi inarejea leo kwa Simba na Namungo Fc zinazocheza mechi za viporo
Ni mchezo ambao vijana wa Didier Gomes wanahitaji kuondoka na alama zote tatu ili kuounguza tofauti ya pointi dhidi ya watani zao Yanga ambao kimahesabu wataondoka kileleni kama Simba itashinda mechi zote tatu za viporo
Simba ilitua mkoani Dodoma jana na jioni wachezaji wakapata nafasi ya kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri mahali ambapo mtanange huo utapigwa
Gomes amesema wabatarajia kuwa na mchezo mwenye ushindani kutoka kwa Dodoma Jiji ambayo haijapoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani lakini lengo lao ni kuhakikisha wanashinda
Wakati Simba ikicheza na Dodoma Jiji, wawakilishi wengine wa nchi katika michuano ya Kimataifa Namungo Fc wao watakuwa jijini Dar es salaam kuikabili KMC