Keshokutwa Alhamisi Februari 04 Simba itashuka uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kuikabili Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Mchezo huo ni miongoni mwa mechi za viporo ambazo Simba inacheza wiki hii
Baada ya kuibuka mabingwa wa michuano ya Simba Super Cup juzi, kocha Didier Gomes aliwapa wachezaji wake mapumziko ya siku moja wakitarajiwa kurejea kambini leo tayari kwa safari ya Dodoma
Baada ya mchezo dhidi ya Dodoma Jiji, Simba iterejea jijini Dar es salaam ambako inakabiliwa na mchezo dhidi ya Azam Fc utakaopigwa Februari 07 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE