Hakuna wa kushindana na Simba kwenye usajili Afrika Mashariki - Magori

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Feb 2021
Hakuna wa kushindana na Simba kwenye usajili Afrika Mashariki - Magori

Afisa Mtendaji Mkuu wa zamani wa Simba, Crescentius Magori, amesema Simba imekuwa kivutio cha wachezaji wengi katika ukanda wa Afrika Masharki na hata kati na kuwa hakuna mchezaji ambaye wao watamtaka atakwenda kusajiliwa na timu nyingine katika ukanda huo

Magori ambaye kwa sasa ni mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, na juzi akitangazwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, amesema hata mchezaji Fiston Abdul Razak aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni sio mchezaji mgeni kwao, kwani angekuwa tayari ameshavaa uzi wa Simba siku nyingi kama wangemtaka

"Fiston nilitaka kumsajili kwenye michuano ya Chalenji liyofanyika nchini Kenya kwenye Jiji la Nairobi na Nakuru. Ile michuano ambayo Zanzibar aliingia fainali mwaka 2017. Alikuja na timu ya Taifa ya Burundi. Tayari tulishakuwa kwenye nafasi nzuri, lakini akapata ofa nono zaidi kwenda nchini Angola, hivyo tukaachana nae," alisema Magori.

Magori alisema hayo baada ya madai kuwa klabu ya Simba imekuwa ikichukua wachezaji ambao timu nyingine zimeshaonyesha nia ya kuwasajili, hivyo kuonekana hawana jicho zuri la kuangalia wachezaji mpaka timu zingine zimtaje.

"Si kweli. Hawa wachezaji wote unaowaona wanacheza humu humu Afrika na sisi tunawaona. Sema sisi huwa hatuongei. Tunaongea baada ya usajili," alisema Magori.

Alisema kuwa hata wachezaji Luis Miquissone kuwa baadhi ya klabu wanadai kuwa walitaka kumsajili, lakini wao wakawahi kitu ambacho si kweli, kwani Miquissone wao ndiyo walioanza kumuona kwenye mechi ya kwanza kati ya Simba dhidi ya UD Songo iliyochezwa nchini Msumbuji na kuanza naye mazungumzo.

"Sisi tulianza kuzungumza naye kabla hata hajaja hapa kwenye mechi ya marudiano. Hata Benard Morrison jina lake nililetewa kabla hajaenda Yanga, lakini tatizo rekodi zikaonyesha kuwa hajacheza muda mrefu, tukasubiri kwanza acheze atakakokwenda kucheza kwa miezi sita ili tumuone kwanza. Yeye mwenyewe aliipenda sana Simba baada ya kuiona ikicheza Simba Day dhidi ya Asante Kotoko mwaka 2017"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’