Gomes asifu kiwango cha wachezaji Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Feb 2021
Gomes asifu kiwango cha wachezaji Simba

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake katika michuano ya Simba Super Cup iliyomalizika jana kwa Simba kuibuka mabingwa

Kupitia michuano hiyo, Gomes amesema ameweza kuwafahamu wachezaji wake wote na vile ambavyo anaweza kuwatumia katika kikosi chake

Gomes amesema timu yake imeonyesha uimara katika safu ya ulinzi lakini pia safu yake ya ushambuliaji ilikuwa bora pamoja na kuwa yapo maeneo ambayo atahitaji kuyafanyia kazi

"Binafsi nimefurahishwa na michuano hii kwani imenipa mwanga wa kikosi changu. Nimepata nafasi ya kufahamu uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na hilo litanisaidia katika kuiandaa timu. Tulikuwa bora katika safu ya ulinzi pamoja na ushambuliaji, ingawa yapo maeneo ambayo tunapaswa kuyafanyia kazi," alisema Gomes

Baada ya michuano hiyo kukamilika, Simba imeanza maandalizi tayari kwa mechi mbili za viporo ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji na Azam Fc

Februari 04, Simba itasafiri mkoani Dodoma kuikabili Dodoma Jiji kisha kurejea jijini Dar es salaa kucheza na Azam Fc Februari 07

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’