Winga Luis Miquissone amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo Jumapili
Miquissone amekabidhiwa kitita cha Tsh Laki Tano baada ya kushinda tuzo hiyo
Hiyo ilikuwa tuzo ya pili mchezaji wa Simba anashinda kwenye michuano hiyo
Kiungo Larry Bwalya aliibuka nyota wa mchezo wa kwanza dhidi ya Al Hilal, mchezo ambao Simba ilishinda kwa mabao 4-1
Hongera kwake, amefanya kazi nzuri sana katika mchezo huo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana
ADVERTISE HERE