Simba imelibakisha nyumbani taji la michuano ya Simba Super Cup licha ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana na TP Mazembe
Ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na sare ya leo,imeifanya Simba ifikishe alama nne
Al Hilal wameshika nafasi ya pili wakiwa na alama tatu wakati Mazembe wamemaliza nafasi ya tatu na alama yao moja
Kwa kiasi kikubwa mashindano haya ambayo yaliandaliwa na Simba, yamefanikiwa
Mabingwa hao wa nchi wamepata radha ya ligi ya mabingwa kabla ya kuanza kwa hatua ya makundi mwezi ujao
Pongezi kwa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez kwa kuja na ubunifu huu ambao hakuna shaka utaendelezwa
Kocha Didier Gomes amepata nafasi ya kuwafahamu vyema wachezaji wake katika mashindano makubwa, sasa limebaki jukumu lake kuunda kikosi chake cha ushindi