Licha ya kulazimishwa matokeo ya suluhu ya bila kufungana dhidi ya TP Mazembe, Simba imefanikiwa kulibakisha nyumbani taji la Simba Super Cup
Mchezo huo wa pili uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, ulikuwa na ushindani mkali Simba ikitengeneza nafasi za wazi zaidi za kufunga
Kiungo Clatous Chama ndiye aliyekaribia kuifungia Simba mipira yake miwili ikigonga miamba na mmoja kuokolewa na mlinda lango



Luis Miquissone, Chris Mugalu nao kwa nyakati tofauti walishindwa kuzitumia nafasi zao kufunga
Ulikuwa mchezo ambao ni kipimo kizuri kwa Simba kuelekea mikiki mikiki ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi ambayo inaanza kutimua vumbi katika kipindi cha wiki mbili zijazo
Simba imefikisha alama nne, wakati Al Hilal ina alama tatu na TP Mazembe wakishika mkia na alama moja
Michuano hii imempa nafasi kocha Didier Gomes kufahamu wachezaji wake na bila shaka amepata mwanga wa kazi anayopaswa kuifanya ili kuhakikisha Simba inafikia malengo yake katika michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika kwa ngazi ya vilabu