Match Day : Simba vs TP Mazembe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Jan 2021
Match Day : Simba vs TP Mazembe

Jioni ya leo Wanamsimbazi wataonja radha halisi ya michuano ya ligi ya mabingwa wakati mabingwa wa Tanzania Simba watakaposhuka uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na mabingwa wa DR Congo TP Mazembe katika mchezo wa kuhitimisha michuano ya Simba Super Cup

Huu sio mchezo wa kukosa kwani kwa hakika utakuwa kipimo sahihi kwa Simba kulekea kampeni yao ya michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi

Simba wenyeji wa michuano hiyo wamepania kulibakisha kombe nyumbani, wakihitaji alama moja tu kutoka kwenye mchezo huo baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa kwanza

TP Mazembe wao walikumbana na kipigo wasichokitarajia kutoka kwa Al Hilal kwa kufungwa mabao 2-1 hivyo ni wazi leo watataka kushinda

Mazembe watahitaji kushinda zaidi ya mabao matatu ili kuweza kuibuka mabingwa wa michuano hiyo ambayo bingwa ataondoka na kitita cha Tsh Milioni 15

Hii ni mechi muhimu sana kwa makocha wa timu zote kupima uimara wa vikosi vyao

Lakini kwa mashabiki huu ni mchezo wa kipekee kushuhudia burudani na ufundi kutoka kwa miamba hawa wa soka

Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi kamili jioni mashabiki wakiaswa kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono klabu yao ya Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Mohammed Dewji 'Mo' ameweka msisitizo kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi ili pamoja na kushuhudia burudani, wachangie mapato ya klabu yao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’