Kikosi cha Simba kinatarajia kushuka dimbani kuwavaa wenyeji wao Gendarmarie Nationale FC katika mchezo wa marudiano wa hatua ya awali ya mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaofanyika leo huko Djibouti.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 10:00 jioni kwa saa za Djibouti, sawa na muda kama huo kwa saa za Afrika mashariki.
Simba watashuka uwanjani wakiwa na mtaji wa mabao 4-0 ambao waliupata katika mechi ya kwanza iliyofanyika Februari 11 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema timu yake itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na lengo moja la kumaliza kazi iliyobaki.
Djuma amesema hakuna timu yenye kuamini imesonga mbele mpaka filimbi ya mwisho itakapopigwa na kujumuisha matokeo ya dakika 180 za hatua hiyo ya awali huku akiongeza sasa wanafaida ya kuwajua wapinzani wao.
Kocha huyo alisema kuwa anaamini kupata ushindi katika mechi ya leo kutawasaidia kujiweka katika nafasi nzuri kwa ajili ya hatua inayofuata na mechi nyingine zinazoendelea za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
"Hakuna anayesema tayari tumeshavuka hatua ya pili, mpira hauko hivyo, tunatakiwa kupambana na kushinda kila mechi iliyoko mbele kwa sababu timu zote zinaingia uwanjani kushindana na si kukamilisha ratiba," alisema kocha huyo.

ADVERTISE HERE