Ujumbe wa Bosi Mo kwa Wanamsimbazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Jan 2021
Ujumbe wa Bosi Mo kwa Wanamsimbazi

Ndugu zangu wana-Simba. Napenda kuwataarifu kwamba sisi katika uongozi wa Simba tumejizatiti na kuweka mikakati ya kuhakikisha tunachukua tena Ubingwa wa Ligi, kuchukua Kombe la FA, na kufika mbali kwenye mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.

Pia tunaendelea na mikakati ya kuhakikisha kwamba Klabu yetu inajenga chapa na sifa bora Afrika na kote duniani. Sehemu ya mkakati huo ni haya mashindano tuliyoandaa ya Simba Super Cup, ambayo hadi sasa yamefanikiwa na yamepokelewa vizuri kote Afrika.

Nia yetu ni kwamba mashindano haya ya Simba Super Cup tuyafanye kila mwaka. Tayari tumeanza maandalizi ya mashindano haya kwa msimu ujao ambapo tutaongeza idadi ya timu kubwa za Afrika. Nia yetu pia ni kwamba mashindano haya yajiendeshe yenyewe kibiashara. Vyanzo vya fedha za kugharamia mashindano haya ni:- wadhamini, malipo ya utangazaji, viingilio na mchango wangu binafsi.

Wito wangu maalum kwenu ni kwamba, ili mashindano yajayo yawe bora zaidi, nawaomba tuje uwanjani, tujaze uwanja kwenye mechi za haya mashindano. Tukija kwa wingi tutakuwa tumefanikiwa mambo manne:- tumechangia klabu yetu kimapato, tumeyapa mashindano haya hadhi na heshima stahili, tumevutia timu nyingine kubwa Afrika ziombe kuja kushiriki, na tumewapa wachezaji wetu moyo na hamasa.

Kwahiyo, nawaomba shime tuje uwanjani kwa wingi kwenye mechi yetu na TP Mazembe siku ya Jumapili, tarehe 31.01.2021. Pamoja na kwamba tunaweza kuitazama mechi kwenye luninga lakini mapato yatakuja Simba, na tutaweza kufanya mambo makubwa zaidi, kama tutakuja mpirani.

Tuonyeshe mapenzi na uzalendo kwa Klabu yetu kwa kuja kwenye mechi. Hii pia itatupa moyo sisi viongozi kuendelea kubuni na kutekeleza mambo makubwa na mazuri zaidi. Shime, tukutane kwa Mkapa Jumapili saa kumi alasiri. Tuma huu ujumbe kwa mwana-Simba mwenzako.

Mohammed Dewji
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi,
Simba Sports Club
30/01/2021

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’