Klabu ya Simba imeweka wazi zawadi atakazopata bingwa wa michuano ya Simba Super Cup iliyoanza Januari 27, 2021 ambazo ni fedha tasilimu shilingi milioni 15, kikombe pamoja na medali.
Taarifa hiyo imetolewa leo kupitia kwa Msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara, ambaye pia amesema baada ya mchezo wa mwisho kutakuwa na tafrija (after party) ambayo itafanyika 'Kidimbwi Beach', jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, Manara amemtangaza msanii wa BongoFleva, Zuchu kuwa mtumbuizaji katika mchezo wa mwisho wa michuano hiyo utakaopigwa Jumapili, Januari 31, 2021 kati ya Simba vs TP Mazembe.
"Mashabiki mfike mapema uwanjani na mjifunze namna ya kucheza sukari", amesisitiza Zuchu ambaye pia amemtaja golikipa Aishi Manula kuwa ndiye mchezaji anayemvutia zaidi kutoka kwenye kikosi cha Simba