Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez ameonyesha kushangazwa na uongozi wa klabu ya Yanga kuendelea kumng'ang'ania Mghana Bernard Morrison ambaye ameonyesha kutokuwa na mapenzi na klabu hiyo
Akizungumza na redio Clouds FM mapema leo, Barbara amesema sakata la Morrison na klabu ya Yanga bado halijamalizika na Wanasheria wa Simba wanaendelea kulishughulikia kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa
Hata hivyo, amesisitiza kwamba hakuna haja kwa Yanga kuendelea kupoteza muda kumng'ang'ania mchezaji ambaye hataki
"Kesi ya Morrison na Yanga bado ipo, wapo Wanasheria wetu wanatusaidia kwenye hiyo kesi. Lakini naona Yanga wanahangaika. Ni kama upo kwenye mahusiano mnaachana halafu bado unamlazimisha mpenzi wako wa zamani arudi"
"Mmeachana, hakutaki, ameshaendelea na maisha mengine, bado unamng’ang’ania wa nini? Halafu mwenzio anamaisha yake hakusubiri. Achananae," alisema Barbara