Mshambuliaji mpya wa Simba, Junior Lokosa amesema anashukuru kujiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara akiahidikuonesha alichonacho kuisaidia kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezaji huyo wa Nigeria aliyewahi kuichezea Esperance ya Tunisia alisema anajua mashabiki wa klabu hiyo wanatarajia mengi kutoka kwake hivyo atajitahidi kuonesha ubora wake.
"Nina furaha kujiunga na Simba kwa sababu ni timu kubwa Afrika, nitajitahidi kufanya nao kazi kuwapa kile kilicho bora ili kuisaidia timu kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika," amesema
Lokosa ametua Simba akiwa mchezaji huru, akisaini mkataba wa miezi sita ambao unaweza kuongezwa mwishoni mwa msimu
Kwa sasa ametua kwa ajili ya mchuano ya ligi ya mabingwa
Akimzungumzia Lokosa, Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema nyota huyo ana uzoefu mkubwa katika soka la Afrika, akiwatumikia Esperance waliotwaa ubingwa wa Afrika kwa misimu miwili mfululizo 2017/18 na 2018/19
Lokosa amepewa program maalum ya mazoezi ili aweze kuwa timamu tayari kuanza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi