Bosi Barbara anazidi kuchanja mbuga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jan 2021
Bosi Barbara anazidi kuchanja mbuga

Moja ya majukumu ya Mtendaji Mkuu wa Taasisi yoyte ni kuhakikisha anaimarisha uchumi wa Taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato

Katika muda mfupi ambao Barbara Gonzalez ametumika kama Mtendaji Mkuu wa Simba, amefanya mambo makubwa yenye faida za kiuchumi kwa Simba

Kila mmoja amepongeza kuanzishwa kwa michuano ya Simba Super Cup ambayo sio tu inainufaisha Simba kiuchumi, lakini pia inakuza 'brand' ya Simba ndani na nje ya Afrika

Barbara ameonyesha dhamira ya kutaka kuipeleka Simba 'next level' kama msemo huo unavyotumiwa na Wanasimba wenyewe

Ndio maana umeona tayari amezitembelea klabu karibu zote kubwa barani Afrika kujifunza mambo kadhaa ambayo anaamini akiyaleta Simba yatakuwa na manufaa

Bosi Lady huyu tayari ametimiza jukumu moja kubwa msimu huu ambalo ni kuiongoza Simba kutinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa

Kutetea ubingwa ligi kuu kwa msimu wa nne mfululizo pamoja na kushinda taji la FA ni vipaumbele vingine alivyodhamiria kuvikamilisha

Tunaona maboresho ya benchi la ufundi, Barbara akishiriki katika kushawishi kupatikana kwa makocha wenye uzoefu na CV kubwa

Itoshe kusema wale waliokuwa wakibeza uteuzi wake mpaka sasa watakuwa wamejifunza kitu, kwani kazi aliyoifanya ndani ya muda mfupi huwezi kulinganisha na kile kilichofanywa na mtangulizi wake Senzo Mbartha ndani ya mwaka mmoja

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’