Mnasema nina 'busha', ndio ninalo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Jan 2021
Mnasema nina 'busha', ndio ninalo

Jana winga Bernard Morrison aliwafunga midomo wakosoaji wake na wale wanaomdhihaki kwenye mitandao ya kijamii

Simba ikipata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal katika mchezo wa ufunguzi wa Simba Super Cup, Morrison alifunga mabao mawili na kusababisha bao moja lililowekwa kambani na Perfect Chikwende

Baada ya kufunga bao lake la kwanza, Morrison 'Mzee wa Kuwakera' akachukua mpira na kuuweka ndani ya 'bukta' yake kuonyesha ishara ya kuwa na 'busha'

Akizungumzia aina hiyo ya ushangiliaji, Morrison alisema kuwa amewasikia mashabiki wanaomkejeli kwenye mitandao ya kijamii kutokana na maradhi ya Hernia yaliyokuwa yakimsumbua

"Mimi sifahamu 'busha' ni nini, lakini naweza kukubali sawa ninalo. Sasa nilitaka kuwaonyesha wale wanaonikejeli kuwa hata kama nina busha lakini halinizuii kufanya mambo yangu uwanjani"

"Hernia ni ugonjwa kama ulivyo ugonjwa mwingine wowote, lakini wapo wanaochukulia jambo hili tofauti," alisema Morridon

Morrison alikuwa bora sana katika mchezo huo ambao alitumika kwa takribani dakika 30 tu

Mashabiki wa Simba walilipuka kwa furaha baada ya kumshuhudia uwanjani, ukiwa umepita muda mrefu tangu nyota huyo alipoonekana kwa mara ya mwisho dimbani

Wakati wa usajiliwa dirisha dogo kulikuwa na tetesi kuwa Morrison angeweza kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wangeachwa lakini kwa hakika nyota huyu aliyetua kutoka klabu ya Yanga bado ni mchezaji muhimu sana

Atakuwa na mchango mkubwa katika michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi itakayoanza mwezi ujao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’