Kiungo maestro Larry Bwalya jana aliibuka kuwa nyota wa mchezo wa kwanza wa Simba Supra Cup dhidi ya Al Hilal uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Simba ikiondoka na ushindi wa mabao 4-1
Bwalya aliondoka na kitita cha Tsh Laki tano akituzwa baada ya kuchaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo
Ndiye mchezaji aliyeonyesha kiwango cha juu zaidi dimbani, aliwan'garisha sana mabingwa hao wa nchi
Bwalya alilikamata dimba, hakika ilikuwa burudani kumtizama akifanya soka lionekane kuwa mchezo rahisi sana
Ni huyu huyu Bwalya ambaye mwanzoni mwa msimu kulikuwa na maswali mengi kama ataweza kumudu ushindani uliopo ndani ya kikosi cha Simba?
Lakini kama umemfuatilia katika michezo ya karibuni, utakubali kuwa Bwalya ameweza kujibu maswali ya wale wote waliokuwa wakitilia mashaka uwezo wake
Msimu huu kiungo Clatous Chama 'CCC' maarufu Mwamba wa Lusaka ndiye aliyezungumzwa zaidi, lakini kwa hakika sasa ufalme wake unaweza kuwa mashakani kama Bwalya ataendelea kubaki katika kiwango alichonacho sasa