FT : Simba 4-1 Al Hilal

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Jan 2021
FT : Simba 4-1 Al Hilal

Simba wametakata uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo wakiwafumua Al Hilal mabao 4-1 katika mchezo wa Simba Super Cup

Ulikuwa ni mchezo ambao Simba ilikuwa bora kwa muda wote pamoja na kuwa walifunga mabao yao matatu katika kipindi cha pili

Larry Bwalya ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huo akiwa mfungaji wa bao la kwanza lakini pia akiwa ndiye injini ya timu katikati ya dimba

Perfect Chikwende, mchezo wa kwanza bao la kwanza leo akiwa na uzi wa Simba. Ndiye aliyeifungia SImba bao la pili akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango wa Al Hilal baada ya shuti la Morrison

Kipindi cha pili kilikuwa cha Bernard Morrison 'BM3' aliyewapa burudani mashabiki wa Simba waliokuwa 'wamemmis' akifunga mabao mawili na kusababisha bao jingine

Pamoja na kucheza chini ya dakika 30, Morrison alikuwa bora kila alipogusa mpira kasi yake iliwapa wakati mgumu walinzi wa Al Hilal ambao walionekana kukata pumzika katika kipindi cha pili

Ushindi huu unaiweka Simba katika nafasi nzuri ya kushinda Super Cup kama watashinda mchezo wao wa pili dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo utapigwa Jumapili Januari 31,  2021

Huu ni mwanzo mzuri kwa Simba ambayo inatumia michuano hii kujiandaa na mshike mshike wa michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’