Dua za Watanzania wote leo ni kwa timu yao iweze kupata ushindi dhidi ya Guinea ili iweze kutinga nusu robo fainali ya michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon
Ni mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi ambao utapigwa kuanzia saa nne usiku
Tanzania yenye alama tatu, ikishinda leo itafikisha alama sita na kujihakikishia kuwa katika nafasi pili za juu na hivyo kutinga robo fainali
Hata hivyo hautakuwa mchezo rahisi mbele wa vinara wa kundi hilo, Guinea wenye alama nne
Kuelekea mchezo huo, Kocha Mkuu wa Tanzania Etienne Ndayiragije amesema wanafahamu hawahitaji matokeo mengine zaidi ya ushindi kuweza kutinga robo fainali
Huu ni mchezo wa kufa na kupona kwao, akiahidi vijana wake kupambana kuwatoa kimasomaso Watanzania
Mech zote mbili zitapigwa saa nne usiku, Zambia ikicheza na Namibia ambao tayari wameyaaga mashindano hayo