Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes atakuwa na nafasi ya kukifanyia tathmini kikosi chake katika michuano ya Simba Super Cup inayoanza kesho Jumatano kwa mchezo kati ya Simba dhidi ya Al Hilal
Gomes aliyetua kuchukua nafasi ya Sven Vandenbroeck, amesema michuano hii itampa taswira ya kikosi chake kabla ya kuanza kuijenga timu yake kimbinu
Aidha Mfaransa huyo amesema Simba wakiwa waandaaji wa michuano hiyo, watapambana kuhakikisha wanashinda
"Tuna mashindano makubwa wiki hii na jina la mashindano ni Simba Super Cup ambayo ni muhimu kushinda, kuongeza kujiamini"
"Itakuwa nafasi kwangu kuwaona wachezaji na kujua uwezo wao na kuandaa mfumo mzuri wa michezo ijayo ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika," alisema Gomes katika Mkutano na Wanahabari mapema leo