Gomes ampa tano Chikwende

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
26 Jan 2021
Gomes ampa tano Chikwende

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amemwagia sifa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Perfect Chikwende kuwa atakuwa msaada mkubwa kwa kikosi cha mabingwa hao wa nchi

Gomes ameeleza kumfahamu Chikwende kabla hajasajiliwa na Simba, uwepo wake Msimbazi utakuwa na faida kubwa kwa timu

"Ni mchezaji anayejituma na kujitolea sana uwanjani, hata hapa katika mazoezini mmemuaona jinsi anavyopambana. Najua hayuko fiti kwa asilimia 100 kutokana na kutocheza mfululizo sababu ya changamoto ya corona lakini naamini atakuwa sawa.

"Nimewaona wachezaji wa Simba wengi wako vizuri sana kiufundi kazi yangu sasa ni kuwaunganisha kimbinu ili tuweze kuwa na timu yenye ushindani zaidi," alisema Gomes aliyetua Simba juzi akitokea klabu ya El Marreikh

Chikwende alisajiliwa na Simba katika usajili wa dirisha dogo akitajwa kuchukua nafasi ya Francis Kahata katika kikosi kitakachoshiriki ligi kuu

Nyota huyu alin'gara katika kikosi cha Fc Platinum kilichokutana na Simba katika raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa

Ndiye aliyefunga bao pekee ambalo liliwapa Fc Platinum ushindi wa bao 1-0 kule Zimbabwe kabla ya kuchezea kipigo cha mabao 4-0 jijini Dar es salaam

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’